Indirimbo ya 205 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Yesu Mwokozi aita kwa pendo mimi na wewe na wote, na yu karibu kukukaribisha wewe uliye dhambini.
Urudi, urudi, Sasa urudi kwa Yesu! Anakuita na anakungoja. Leo urudi kwa Yesu!
2
Mbona kukawa anapokuita? Anakungoja, ufike! Kuna nafasi karibu na Yesu; njia ni wazi kwa wote.
3
Nyakati zetu zapita upesi, hazitarudi kabisa. Njoo kwa Yesu upate amani, leo ungali mzima!
4
Ona upendo mkubwa wa Yesu, unaenea kwa wote! Na kwa neema anakukumbuka wewe na mimi na wote.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 205 mu Nyimbo za wokovu