Indirimbo ya 50 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Sitasumbuka kwa kuwa Mungu ananitunza daima, anachukuwa mizigo yangu nyakati zote za mwendo.
Sijaiona nyingine siku, na jana imetoweka, na leo Mungu anazijuwa hitaji zote ninazo.
2
Sitasumbuka kwa kuwa Mungu ni baba yangu kabisa. Hawezi kunisahau mimi ingawa akijificha.
3
Sitasumbuka kwa kuwa Mungu anishibisha neema, anipa yote yanifaayo kwa roho yangu na mwili.
4
Mauwa yote anayavika, Na ndege wote wa anga wanapokea chakula chao pasipo shamba na ghala.
5
Ninafurahi katika Bwana, Na kama ndege naimba. Najuwa kwamba nyakati zote babangu ananitunza.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 50 mu Nyimbo za wokovu