Indirimbo ya 206 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Rafiki yangu, tazama, wapita njia ya wapi? Milele, je? utakaa wapi ukikataa Mungu?
Ujiandae sasa, utakutana na Mungu! Lazima uwe tayari kwa sababu utamuona!
2
Dunia haina raha, amani wala salama. Fahari yake ikikuloga, utapotea njia.
3
Lo! Yesu anakuita! Kwa nini unachelewa? Ushike njia ufike kwake! Ataja jina lako.
4
Uache haya na hofu, Mwokozi anakupenda! Kwa damu alikomboa wewe, anakutaka sasa.
5
Ikiwa unachelewa kupatanishwa na Mungu, utamkuta Mwokozi kama mwamuzi mwenye haki.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 206 mu Nyimbo za wokovu