Indirimbo ya 14 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Mwokozi wangu ulikwenda juu kukaa kuumeni kwake Baba; Utakusanya sisi sote huko, mbinguni kwako, utatufikishsa. :/: Makao mema wa’tuandalia, unatungoja kwake Mungu Baba. :/:
2
Mwombezi wetu wewe, Yesu Kristo, kwa’jili yetu mbele yake Baba. Wachunga sana sisi, kundi lako, na watusaidia ‘jaribuni. :/: Na siku zote unatuombea, watushindia vita kali huku. :/:
3
Mikono yako uliwanyoshea walio wako, siku uli’kwenda; na hivyo siku utakaporudi utabariki wakuaminio. :/: Ulivyokwenda, utakavyorudi; niombe nikakeshe kwa imani!. :/:



Uri kuririmba: Indirimbo ya 14 mu Nyimbo za wokovu