Indirimbo ya 145 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Mungu wangu mkuu, wanijaza mwenyewe, na uzima u katika wewe. Nina raha moyoni na amani halisi, ninaishi katika upendo.
2
Sasa ninakusifu wewe, Yesu Mwokozi, unakaa rohoni daima. Kila ‘nachohitaji wanijaza kwa pendo. Wewe yote, na mimi si kitu.
3
Jina lako ni pendo, kulijua hakika kunafanya safari nyepesi. Mimi mtu dhaifu, ila kwako ni nguvu; niongoze katika safari!
4
Mbele ya uso wako giza yote yatoka; nuru inaangaza moyoni. Yamepita ya kale, sasa yote ni mapya. Ni maisha ya heri ajabu!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 145 mu Nyimbo za wokovu