Indirimbo ya 295 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
E’, furahini watu wake Mungu! Mwokozi wetu alituokoa. Neema kubwa, pendo la ajabu! Tusifu Mungu sana siku zote!
E’ Mungu ana mamlaka yote, ni ngao na makimbilio yangu; Ni Baba yangu, na anasikia maombi yangu. Asifiwe!
2
E’, furahini watu wake Mungu! Tuimbe nyimbo za furaha nyingi! Tusiogope ila tumwamini na twende mbele kwa uweza wake!
3
E’, furahini watu wake Mungu! Tukimahangilia (sic) Mungu wetu, jirani zetu wasioamini watatamani kumjua Yesu.
4
E’, furahini watu wake Mungu! Mfalme wetu yu pamoja nasi. Kitambo bado- na tutahamia mbinguni kwake Mkombozi wetu.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 295 mu Nyimbo za wokovu