Indirimbo ya 281 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Yote ninayo niliyapokea kwa wema wake unaonea. Namsifu Yesu, namtegemea, aliniokoa kwa neema.
Niliyekuwa nimetoroka, kwa pendo lake nimeokoka. Yesu yu mwema na mwenye rehema, nimeokolewa kwa neema!
2
Nilitembea zamani dhambini katika njia ya kufa, lakini Yesu alinitafuta porini, akaniokoa kwa neema.
3
Natakasiwa na Yesu Mwokozi, si kwa majuto na si kwa machozi, bali kwa damu, ninao ‘kombozi; nimeokolewa kwa neema.
4
Raha ya mbingu imeniingia, kwa shangwe kubwa ninafurahia Yesu, kwa kuwa anirehemia; nimeokolewa kwa neema.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 281 mu Nyimbo za wokovu