Indirimbo ya 265 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Tu wasafiri, twakaribia nchi ya mbingu kwa Mungu baba. Tusiogope bonde la kufa, Yesu atuongoza kwake!
:/: Tu wasafiri:/: tutakutana nyumbani mwa Baba. E’ Bwana Yesu utuongoze, tufike sote mbinguni!
2
Wengi katika wapendwa wetu wamevuka mto wa kufa. Walifuata mwito wa Mungu. Wakahamia nchi nzuri.
3
Katika mwendo wa duniani walitazama Mwokozi wao, na waliacha mambo ya huku, walipendeza Bwana Yesu.
4
Ndugu wapendwa, tuendelee, hata ikiwa shida njiani! Yesu ni njia, kweli, uzima; tumfuate siku zote!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 265 mu Nyimbo za wokovu