Indirimbo ya 139 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Nina furaha kubwa, napumzika sana, kwa kuwa nimefika kwa Mungu, Baba yangu. Ameniweka huru na mbali na utumwa, na sasa nakaa salama.
2
Zamani nilidhani kuacha dhambi zote, lakini sikuweza kushinda peke yangu. Ninamwamini sasa Mwokozi wangu, Yesu, na yeye ananishindia.
3
Mwokozi wangu, Yesu, aliyenifilia, aliokoa mimi, angali anipenda; nahesabiwa haki katika damu yake, inayosafisha kabisa.
4
Na nikijaribiwa na mwili wangu tena, ninakumbuka Yesu, apita vitu vyote. Neema yake kubwa kuliko dhambi zangu. Ninamshukuru Mwokozi.
5
Na sasa Bwana Yesu akaa ndani yangu, neema yake kubwa yanizunguuka mimi. Sitasumbuka tena, nimejiweka kwake, na Mungu anilinda vema.
6
Shetani akitaka kufanya vita sasa, sitaogopa yeye na mamlaka yake. Maneno yake Mungu, ni yenye nguvu sana kwa wote wanaoamini.
7
Ninaenenda sasa kwa jina lake Yesu, salama nitafika nyumbani mwa Babangu. Lakini safarini naimba siku zote, nikimshukuru Mwokozi.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 139 mu Nyimbo za wokovu