Indirimbo ya 78 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Nina uzima wa milele, na tumaini ni imara, mbinguni nitaona Yesu, Mwokozi wangu kwa furaha.
2
Nina urithi bora huko unaolindwa hata mwisho. Na kila siku ya jaribu natiwa nguvu naye Baba.
3
Namshukuru Mungu wangu! Ananitunza siku zote katika shida na taabu, kwa hiyo sisumbuki tena.
4
Rohoni mwangu ni amani, naimba kwa furaha kubwa. Nikiongozwa naye Yesu naendelea kwa salama.
5
E’ Bwana Yesu, unifunze ku’tumikia wewe vema wakati ubakio tena wa mwendo wangu dunianai!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 78 mu Nyimbo za wokovu