Indirimbo ya 199 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Njoni wote mteswao! Wote wenye sikitiko kwa ajili ya makosa, mje sasa kwa Mwokozi! Kwake mtaona raha, utulivu na amani. Matulizo mioyoni mtapata kwake Yesu.
2
Hataacha sikitiko kulemea moyo wako; Yesu ni mchunga mwema, akuficha mazizini. Pendo lake lina nguvu, huchukua masumbuko, hufariji roho yako, hukutwaa kwake Mungu.
3
Yesu kama nyota nzuri ing’aayo asubuhi, mtu amfuataye ataona njia wazi. hata nyota za mbinguni zikiteketea zote, nyota hiyo ya milele haitazimika kamwe.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 199 mu Nyimbo za wokovu