Indirimbo ya 61 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Enyi watu wa Sayuni, kundi dogo la Mwokozi, Yesu aliwanunua kuwa mali yake Mungu. Sasa mnapita njia ya miiba na hatari kati’ nchi ya ugeni; bali mbingu mtafika.
2
Kumwamini, kumpenda Yesu ni uheri wetu; amri zote zinashikwa kwa upendo na amani. Kwa imani twaokoka, pendo ni uzima wetu. Yesu utusaidie, utujaze pendo lako!
3
Juu ya msingi huo, Yesu, unijenge mimi, na zaidi niungane nawe na kanisa lako! Sisi tu matawi yako, tushirikiane sana, na katika kundi nzima iwe nia moja kweli!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 61 mu Nyimbo za wokovu