Indirimbo ya 154 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
E’ rafiki, shaka zako zipeleke kwako Yesu! Aliyemwamini yeye hataona haya kamwe.
Naamini, naamini, ninakuamini, Yesu. Naamini, naamini, naamini neno lako.
2
Dhambi zote ziungame na kwa damu utakaswe, akuvike haki yake! Atakufikisha kwake.
3
Masumbuko yako yote uyaweke mbele yake! Ukipita uvulini, Bwana Yesu yupo nawe.
4
Na furaha yako pia ijulike kwake Yesu, Yeye, Bwana ju’ ya yote, akubarikie yote!
5
Ujitoe kwake Yesu: Roho, mwili na akili! Vyote vya maisha yako anataka ku’takasa.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 154 mu Nyimbo za wokovu