Indirimbo ya 215 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Mwenyezi Mungu anafanya ishara kubwa duniani, anaondoa minyororo inayofunga watu huku. Avunja nyavu za shetani, na wakosaji waokoka.
2
Maneno yake yana nguvu kushinda yote ya zamani. Na watu wanapiga mbio kuomba ne’ma ya Mwokozi. Wakiyapata masamaha, waimba wote: “Sifu Mungu!”
3
Tazama, ndugu wengi sana wanafuata Yesu leo; katika kila nchi sasa maelfu wanapenda Mungu. Wengine wanavutwa naye Mwenyezi Mungu, Baba yetu.
4
Inua macho, mvunaji, mavuno yanaiva sana! Uende kutafuta watu, uwapeleke kwake Yesu! E’ ndugu wote, amkeni, ‘kawaokowe wenye dhambi!
5
Wengine wanapoingia ufalme wako, Yesu Kristo, nisibakie huku chini, neema hiyo nakuomba! Nakaa mikononi mwako, unifikishe huko kwako!
6
Najua siku ni karibu Mwokozi atakaporudi, awachukue watu wake mpaka nchi ya amani. E’ siku ya uheri bora, nakutamani. Uje mbio.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 215 mu Nyimbo za wokovu