Indirimbo ya 207 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Umgeukie Mwokozi, jitenge na ovu na dhambi! Babako angoja ufike; usiangamie milele!
2
Kijana, unafurahia maisha na mambo ya nchi. Baada ya muda kitambo utahukumiwa na Mungu.
3
Kwa nini kujiangamiza katika tamaa za huku? Usijipoteze dhambini! Dunia isikuharibu!
4
Umkimbilie Mwokozi, atakupokea kwa pendo, na utaokoka hakika kwa nguvu ya damu ya Yesu!
5
Walio mbinguni waimba, wanayo mavazi meupe; hutaki sehemu pamoja na wao nyumbani mwa Baba?
6
Je, mwisho utaona wapi mahali pa kujisitiri? Dunia itakapochomwa utakosa makimbilio.
7
Ujipatanishe na Mungu, na usichelewe, rafiki! Ukimkataa Mwokozi, utatupwa nje gizani.
8
Chagua pasipo kukawa! Mwokozi atakupokea. Angoja ufike kutubu; atakutakasa kwa damu.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 207 mu Nyimbo za wokovu