Indirimbo ya 57 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Yesu, uliyekufa kwa ajili yangu, ninajitoa kwako, niwe mali yako! Bwana, nivute kwako, nifaamishe pendo, niwe dhabihu hai katika shukrani!
2
Yesu, nafika kwako, kao la rehema; Bwana, nitie nguvu kwa neema yako! Niuchukue tena kwa radhi msalaba, ni’tumikie wewe, Mkombozi wangu!
3
Bwana, uniumbie moyo haki, safi, kwako niishi tena hata kufa kwangu! Niwatafute wenye dhambi na udhaifu, niwapeleke kwako, Bwana wa upendo!
4
Vyote ninavyo huku nimepewa nawe, ukivitaka, Bwana, uvitwae vyote! Nina urithi wangu kwako mbinguni juu, nitakuona huko kwa furaha kuu!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 57 mu Nyimbo za wokovu