Indirimbo ya 95 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Nchi nzuri yatungoja huko juu ya mawingu, watakapokusanyika wateule. Siku zina’tubakia zinapita mbio sana; waminifu watarithi nchi nzuri.
:/: Lo! Ufalme wake Mungu u karibu!:/: Uwe safi, roho yangu, ukakeshe siku zote! Lo! Mfalme wake Yesu yu karibu!
2
Twaamini tutaona nchi ile kwa uwazi, tunangoja sana Mkombozi wetu; kwa dalili tunaona siku yake ni karibu; zinatuarifu Yesu aja hima.
3
Maandiko yanasema: Mkombozi atakuja, katika mawingu ataonekana. Haleluya! Haleluya! Atafunga yule mwovu, aliyejaribu kutuangamiza.
4
Katika kungoja Yesu watu wengi wamechoka; waamshe, uwaonye kwa dalili! Kwani neno lake Mungu latimizwa mbio sana, tunaona kwamba yesu yu karibu.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 95 mu Nyimbo za wokovu