Indirimbo ya 193 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Ni neno zuri la ‘aminiwa, listahililo kukubaliwa, ya kwamba Yesu alitujia awaokoe wenye makosa.
2
Wa kwanza mimi wa wenye dhambi, lakini ninafurahi sasa sababu Yesu, Mwokozi wangu, aliniosha kwa damu yake.
3
Mwokozi wetu yu nasi hapa, atenda kazi kwa nia yake; awasha moto rohoni mwetu, uwezo gani utampinga?
4
Viziwi wanasikia sasa, viwete wanatembea sawa, wenye ukoma watakasika, Injili yake yahubiriwa.
5
E’ Bwana Yesu, tupulizie, tujaze Roho Mtakatifu! Uwaamshe waliokufa katika dhambi, uwaangaze!
6
Fungua mbingu unyeshe mvua panapo kiu na jangwa tupu! Uligeuze, likachanue na kufurahi kwa shangwe kuu!
7
Na mataifa wakusujudu mahali pako patakatifu! Amina. Wako ni utukufu na sifa zote! Haleluya!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 193 mu Nyimbo za wokovu