Indirimbo ya 342 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Nasikia habari ya mji Uko mbali na mji na taabu, Nuru yake ni Mwana Kondoa. Siku moja nitaingiamo. Haleluya naruka kwa shangwe Haleluya nakwenda kwa mji, Haleluya nafika upesi Siku moja nitaingiamo.
2
Kuna nchi pasipo machozi Na taabu na vita huzuni, Wala ‘gonjwa hautakuwepo. Siku moja nitaingiamo Haleluya naruka rohoni. Haleluya nakwenda kwa mji, Haleluya karibu kufika Siku moja nitaingiamo.
3
Na jamaa ya nchi ya Heri Wanavikwa na nguo nyeupe, Wana taji za dhahabu safi Siku moja nitakuwako. Haleluya mashaka hayako Wala shida anguko si huko Natamani kuingiamo.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 342 mu Nyimbo za wokovu